Serikali yatoa shilingi bilioni tatu kuwalipa wahudumu wa afya ya jamii

Tom Mathinji
1 Min Read
Serikali yazindua hazina ya shilingi bilioni 3 za malipo kwa wahudumu wa afya kwa jamii.

Serikali siku ya Ijumaa, ilizindua hazina ya shilingi bilioni tatu, itakayotumiwa kuwalipa wahudumu wa afya ya kijamii kote nchini, ambao wamehudumu kwa muda wa miezi minne sasa kote nchini.

Hadi kufikia sasa, zaidi ya wakenya milioni 13 wamenufaika na huduma za afya zinazotolewa na wahudumu wa afya ya jamii, ambao serikali imewapeleka katika vijiji vyote kote nchini.

Akzindua hazina hiyo katika makazi yake rasmi ya Karen Jijini Nairobi, Naibu Rais Rigathi Gachagua aliwapongeza wahudumu hao 107,000 wa afya ya jamii, akiwataja mashujaa ambao wanafanikisha utekelezwaji wa mpango wa afya kwa wote.

“Nyinyi ni nguzo muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa afya ya msingi. nyinyi ni mashujaa hasaa baada ya kufanya kazi hii kwa miaka mingi bila kutambuliwa na serikali. Utawala wa Kenya Kwanza ndio wa serikali ya kwanza kuwatambua. Tunafurahia kujitolea kwenu kuwasaidia wakenya,” alisema naibu huyo wa Rais.

Kwa upande wake,waziri wa afya Susan Nakhumicha,alisema mpango huo ni mhimili mkubwa unaolenga kufanikisha huduma ya afya kwa wote humu nchini.

Wakati huo huo, aliwahimiza wahudumu hao kufanya bidii  kuhakikisha uwepo wa jamii iliyo na afya bora.

Share This Article