Serikali yatoa shilingi bilioni 3.4 kwa mradi wa inua Jamii

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imetoa shilingi bilioni 3,492,591,500 kwa mradi wa inua jamiii katika mwezi wa Septemba.

Wizara ya leba na ulinzi wa jamii imesema hela hizo zinalenga kuwakidhi Wakenya 1,739,919 ambao wamejisajili kwenye mpango huo.

Katib wa ulinzi wa jamii Joseph Motari amesema hela hizo zinajumuisha miradi ya lishe bora huku Wakenya 22,217 wakisajiliwa.

Kila aliyesajili kwa mpango huo atapokea malipo ya shilingi 2,000 za mwezi Septemba.

Motari alitoa hakikisho la kuwa malipo hayo yatakuwa yakitolewa kwa wakati, ili kuwafaidi wanaolengwa.

Share This Article