Serikali yatoa shilingi bilioni 21.8 kufadhili elimu kwa muhula wa tatu

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais William Ruto katika shule ya msingi ya Kikuyu Township, kaunti ya Kiambu.

Serikali imetangaza kutoa shilingi bilioni 21.8 kufadhili elimu ya bure kwa shule za msingi na elimu ya bure ya shule za kutwa za sekondari, kwa muhula wa tatu utakaofunguliwa wiki ijayo.

Kiwango hicho kimetengwa kwa mafungu matatu ikiwa ni shilingi bilioni 14 kugharamia masomo ya bure kwa shule za kutwa za upili,shilingi bilioni 6.1 kwa kwa elimu ya bure kwa shule za kutwa za Junior Seciondary na bilioni 1.6, kugharamia elimu ya bure kwa shule za msingi.

Waziri Ogamba amesema hela hizo zimetolewa ili kuruhusu ufunguzi wa shule kote nchini Jumatatu ijayo Agosti 26 bila tashwishwi.

Ogamba amewataka Walimu wa shule za umma kuhakikisha matumizi ya hela hizo kwa uadilifu akiahidi kukabiliana vikali na watakaofuja pesa.

Hata hivyo kungali na hali ya atiati kuhusu ufunguzi wa shule za umma baada ya miungano ya Walimu KUPPET na KNUT, kutangaza migomo ya kitaifa wakitaka nyongeza ya mishahara miongoni mwa matakwa mengine.

Share This Article