Serikali yatoa mwongozo wa mazungumzo na vijana wa Gen Z

Dismas Otuke
1 Min Read
Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei

Serikali imetoa mwongozo wa mazungumzo ya kitaifa pamoja na vijana wa Gen Z, kutafuta suluhu kwa maswala waliyoaibua wakati wa maandamano yao ya kitaifa maajuzi.

Kwenye taarifa iliyotumwa na Mkuu wa Utumishi wa umma Felix Kosgei, serikali itabuni kamati ya kitaifa ya watu 100  watakaowakilisha  sekta mbalimbali na makundi tofautio ya kijamii.

Kosgei ameyataka makundi hayo yanayojumuisha vijana,wanafunzi wa vyuo vikuu,makundi ya kijamii,wafanyabiashara,baraza la magava na wasomi kuwateua waakilishi wawili kila mmoja kwenye  kamati hiyo, ambayo pia itawajumuisha kiongozi wa wengi na wachache bungeni.

Maswala yatakayojadiliwa na kamati hiyo ni pamoja na nafasi za kazi na fursa nyinginezo,sera ya kitaifa kuhusu shuru,deni la kitaifa,uwakilishi na uwajibikaji,kupambana na ufisadi na mada nyinginezo muhimu.

Kamati hiyo itazuru kaunti zote 47 humu nchini kusikiliza maoni ya makundi mbalimbali kutoka viwango vya wadi na kuwasilisha ripoti kwa Rais ifikiapo Julai 7 mwaka huu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *