Serikali imetetea uamuzi wake wa kuwapeleka wahudumu wa afya wa Kenya kufanya kazi nchini Uingereza.
Akiitetea hatua hiyo, Waziri wa Afya Susan Nakhumicha amesema mkataba wa ushirikiano katika maswala ya kazi kati ya nchi hizo mbili umechangia pakubwa katika ustawi wa sekta ya afya hapa nchini.
Waziri alisema hayo alipowaaga wauguzi 76 wa Kenya kwenda nchini Uingereza.
Aliwapongeza wauguzi wa hapa nchini kwa kujitolea kazini akisema wao ni kiungo muhimu kwa sekta ya afya.
Nakhumicha aliwatakia wauguzi hao kila la heri katika kazi yao mpya.
Mkataba huo wa ushirikiano wa kikazi unatoa fursa ya kubadilishana ujuzi katika maswala ya afya, kando na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.