Wizara ya Michezo imetenga shilingi milioni 190 kuimarisha mipangailio ya riadha ya vijana nchini kupitia kwa mpango maalum wa Talanta Hela.
Waziri wa Michezo Ababu Namwamba amesema kuwa kiwango hicho cha pesa kitagawanywa kwa kambi 41 za riadha zilizoteuliwa kote nchini, huku kambi chache zikitengwa kutoa mafunzo ya mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji.
Kulingana na Waziri mbinu hiyo itahakikisha Kenya inarejesha hadhi yake kimataifa katika shindano hilo.