Wizara ya Ardhi na Nyumba imetangaza awamu ya kwanza ya kuuza miradi 21 ya nyumba 4,888 za gharama nafuu zinazokaribia kukamilishwa kujengwa.
Nyumba hizo ni zile za chumba kimoja, vyumba viwili, na vyumba vitatu.
Taarifa kutoka Idara ya Ujenzi wa Nyumba za Gharama Nafuu imesema kuwa awamu ya kwanza ya nyumba hizo imetengewa Wakenya wanaopata mshahara wa chini ya 20,000 kwa kila mwezi na wanaoishi katika mitaa duni.
Awamu ya pili ya nyumba hizo ni kwa ajili ya wafanyakazi wa kiwango cha kadri wanaopata mshahara wa kati ya 20,000 na 149,000.
Hata hivyo, hakuna mtu ataruhusiwa kununua nyumba mbili.
Wanaotaka kununua nyumba hizo ni sharti wajisali katika mtandao wa Boma yangu kupitia kwa e-Citizen na wawekeze kiwango cha pesa kinachohitajika kununua nyumba hizo.
Nyumba hizo ni zile za miradi iliyo katika kaunti za Machakos, Murang’a, Kirinyaga, Laikipia, Nyandarua, Wajir, Isiolo, Kakamega, Vihiga, Migori, Bomet, Uasin Gishu, Nandi, Nakuru, Kiambu, Embu, na Nyandarua.
Katika mpango wa kwanza wa nyumba zilizotengewa Wakenya wa kipato cha chini, vyumba vya ukubwa wa kilomita 20 mraba vinauzwa kwa shilingi 640,000 na kiwango kingine cha shilingi 3,900 kila mwezi.
Vyumba vyenye chumba kimoja vyaa ukubwa wa kilomira 30 mraba vinauzwa kwa shilingi 960,000 na kiwango cha 5,350 kila mwezi huku kile cha vyumba viwili vyenye ukubwa wa kilomita 40 mraba vikiuzwa kwa shilingi miliomi 1.28 na ada ya shilingi 6,800 kila mwezi.
Katika kitengo cha pili cha wafanyakazi, chumba cha kilomita 20 mraba kinauzwa kwa shilingi 640,000 na 3,900 kila mwezi.
Chumba kilicho na chumba kimoja cha kilomita 30 mraba kinauzwa kwa shilingi 960,000 na malipo ya 5,350 kwa mwezi huku kile cha vyumba viwili cha ukubwa wa kilomita 40 mraba kikiuzwa kwa shilingi milioni 1.28 na malipo ya 6,800 kila mwezi.