Serikali imepiga marufuku mara moja safari zisizo za lazima kwa watumishi wote wa umma, kama nji moja ya kupunguza matuzimishi ya pesa .
Kulingana na arifa iliyotolewa na Mkuu wa Utumushi wa umma Felix Kosgei, safari zilizopigwa marufuku ni zile za:-
a) Kujifunza na masomo ,mafunzo ya kuongeza ujuzi,utafiti na mikutano ya masomo
b) Kongamano,mikutano ya ushirikishwaji,maonyesho na mikutano ya vyama.
Pia kwa safari zinazogharamiwa na waandalizi ambazo huitaji mwajiri kulipia robo ya marupurupu zimefutiliwa mbali.
Taarifa hiyo imeagiza watumishi wa umma wanaopanga kusafiri kuhudhuria vikao vya kuweka mikakati kutumia mikutano ya mitandaoni.
Hata hivyo kwa safari zilizo za lazima kwa watumishi wa umma watahitajika :-
a)Kutafuta kibali kwa wizara wa mambo ya kigeni ili wakenya walio katika mataifa ya kigeni katika sekta husika wajukumiwe.
Safari za kigeni zilizoidhinishwa ni zile ambazo ni lazima kwa serikali ya Kenya kuhudhuria au ni sehemi ya majukumu ya viongozi wa Kenya kuhudhuria.
Pia maafisa wakuu serikalini wamewekewa vikwazo vya usafiri ambapo kwa ziara ya mawaziri nje ya nchi haipaswi kuwa na zaidi ya maafisa watatu akiwemo waziri, huku makatibu wa wizara wasipitishe watu wawili akiwemo katibu
Pia Mawaziri na Makatibu kutoka wizara moja hawataruhisiwa kuwa nje ya nchi kwa wakati mmoja .
Safari za magavana pia hazitazidi watu watatu akiwemo gavana wanaosafari kwa wakati mmoja.
Agizo hilo pia limeweka bayana kuwa hakuna afisa yeyote wa serikali ambaye atapewa ziara ya ugenini kwa zaidi ya siku 7 ikiwemo siku za usafiri.
Kama njia moja ya kupunguza matumizi ya pesa za serikali,Kosgei ameagiza wizara ya hazina kuu kupunguza safari zote za humu nchini na ughaibuni kwa asilimia 50.