Wizara ya Elimu imepiga marufuku mitihani ya mwigo katika shule zote, kama njia moja ya kuzuia vurumai ambazo hushuhudiwa muhula huu wa pili.
Katibu mkuu wa Elimu Belio Kipsang ameagiza shule zote nchini kujitenga na mitihani ya mwigo ambayo huwatia wanafunzi kiwewe na kuishia migomo.
Kipsang ametoa agizo hilo kuzingatia mapendekezo ya kamati ya bunge kuhusu elimu.