Katika juhudi za kuimarisha sekta ya kilimo hapa nchini, serikali imeondoa ushuru wa vyakula vya mifugo na bidhaa zinazotumiwa kutayarisha vyakula hivyo kama vile maharagwe ya soya na mahindi ya njano pamoja na bidhaa zingine.
Akitoa tangazo hilo katika kaunti ya Meru katika ziara kwa wakulima, waziri wa kilimo Mithika Linturi, alisema hatua hiyo pia inalenga kuwavutia wakenya wengi hususan vijana kuingilia shughuli za Kilimo.
Bei ya juu ya vyakula vya kilimo, imetajwa kuwa kikwazo kikuu kwa wafugaji wengi hapa nchini.
Kulingana na Linturi, kilimo hutoa nafasi kubwa ya ajira hapa nchini na kwamba serikali imeimarisha taasisi za kifedha kama vile shirika la mikopo kwa wakulima AFC kwa riba ya chini.