Serikali imeondolea hofu ya kuwepo kwa vyeti ghushi vya umiliki wa ardhi licha ya kutoweka kwa karatasi za kuchapisha vyeti hivyo kutoka kwa afisi ys serikali ya kuchapisha karatasi.
Kulingana na taarifa kutoka wizara ya ardhi,vyeti vyote halali vya umiliki wa ardhi huchapishwa katika wizara hiyo na kuwekwa mihuri baada ya kuthibitishwa.
Wizara hiyo imesema imeweka mikakati ya kukabiliana na ufisadi na kughushi stakabadhi za umiliki wa ardhi, ili kupunguza na hatimaye kuzuia unyakuzi wa ardhi .
Karatasi 367 za kuchapisha vyeti vya kumiliki ardhi zilitoweka kutoka kwa afisi ya serikali ya kuchapisha vyeti vya kumiliki ardhi hali ambayo imezua hofu,huku na tayari mhusika mkuu akitiwa nguvuni kusaidia kwa uchunguzi.
Nambari za usajili wa karatasi hizo ni 5253001 hadi 525300367 na tayari nambari hizo zimefutiliwa mbali.