Serikali yalaumiwa kwa kutelekeza vituo vya mpakani vya Busia na Malaba

Tom Mathinji
1 Min Read

Kamati ya bunge la seneti kuhusu biashara imeikosoa serikali kwa kupuuza shughuli ya utoaji huduma katika vituo vya mpakani vya Malaba na Busia, licha ya pesa nyingi zinazokusanywa kwenye vituo hivyo.

Seneta wa Busia Okiya Omtata, mwenzake wa Kiambu Karungo wa Thang’wa na Crystal Asige, walizuru vituo hivyo vya mpakani kutathmini jinsi serikali itakavyoboresha huduma zake katika vituo hivyo ili kuongeza mapato.

Licha ya vituo hivyo vya Malaba na Busia kuzalisha shilingi bilioni 10 kila mwaka, bado vinakabiliwa na changamoto mbali mbali zinazosababisha msongamano wa magari wa hadi kilomita 20.

Kulingana na kamati hiyo, kuwekwa kwa malango ya kisasa ya mpakani kutasaidia kusuluhisha msongomano huo.

Kuanzia kwa paa zinazovuja, ukosefu wa nguvu za umeme mara kwa mara, ukosefu wa maji, hali duni ya usafi na upungufu wa wafanyakazi, ni miongoni mwa maswala yanayodumaza utendakazi kazi Katika vituo hivyo na kusababisha kupotea kwa kiwango kikubwa cha mapato.

Kamati hiyo ilisema serikali ya Kenya inafaa kushauriana na serikali ya Uganda, ili kusuluhisha tatizo hilo ambalo limeisababisha Uganda kuamua kufanya biashara hiyo ya uchukuzi wa bidhaa na Tanzania.

TAGGED:
Share This Article