Serikali yahaha kuhusu rundo la migomo inayonukia

Dismas Otuke
1 Min Read
Chama cha KUPPET kimesema kitaendelea na mgomo.

Huduma katika afisi za umma huenda zikatatizika  kufuatia arifa kadhaa za migomo zilizotangazwa na vyama vya wafanyikazi wa umma   kuanzia wiki ijayo.

Muungano wa wafanyikazi wa serikali ulitangaza kuwa utaitisha mgomo wa kitaifa na kulemaza huduma zote za serikali, endapo awamu ya pili ya makubaliano ya nyongeza ya mshahara iliyopaswa kuanaza kutekelezwa Julai mosi mwaka huu haitatekelezwa.

Kulingana na Katibu Mkuu wa muungano wa wafanyikazi (UKCS) Tom Odege ambaye pia ni Mbunge wa Nyatike, hawana budi kugoma kuanzia Septemba ,ikiwa hawatapokea nyongeza ya mshahara.

Mgomo huo utaathiri huduma katika vyuo vikuu vya umma kote nchini

Mgomo huo ni wa hivi punde kutangazwa baada ya wahadhiri wa vyuo vokuu vya umma kutoa ilani ya mgomo wao,pamoja na vyama vya walimu wa shule za msingi na sekondari kuapa kutorejea shuleni wiki ijayo, hadi serikali itekeleze nyongeza ya mishahara kikamilifu.

Chama cha wamiliki wa Matatu nchini pia kimetangaza mgomo wa kitaifa kuanzia Jumatatu ijayoi Agosti 26, wakitaka serikali iangzie changamoto zinazokabili sekta ya uchukuzi .

Share This Article