Serikali yafurahia Qatar kuwekeza katika sekta muhimu nchini

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali ya Kenya imeelezea kufurahia kwake kutokana na dhamira ya Qatar kuwekeza katika sekta muhimu nchini kama vile mafuta, gesi na mbolea wakati nchi hizo mbili zikifanyia kazi upanuzi wa sekta za biashara na uwekezaji. 

Kenya na Qatar zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu na zimekusudia kuimarisha uhusiano huo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Biashara Salim Mvurya alipotembelewa afisi mwake na Balozi wa Qatar humu nchini Mohammed Muitar al Enazi.

“Tulijadili umuhimu wa kuanzisha mpangokazi madhubuti wa ushirikiano ambao utaimarisha nyanja za pande mbili za uwekezaji ambazo zitaongeza uhusiano wa kibaishara kati ya Kenya na Qatar,” alisema Waziri Mvurya baada ya mkutano baina yao.

 

Share This Article