Serikali imeanzisha mazungumzo na wahadhiri, wanafunzi, na wafanyikazi wa chuo kikuu cha kiufundi cha TUK ili kumaliza mgomo unaoendelea.
Katibu wa elimu ya juu na utafiti Dkt. Beatrice Inyangala, amesema mazungumzohayo yanalenga kutafuta njia mwafaka ya kumaliza mgomo huo bila kuathiri shughu muhimu chuoni humo.
Aidha, Inyangala amewataka wanafunzi na wazazi kuwa na subira wakisuluhisha mzozo huo.
Mgomo huo ulioanza yapata wiki tatu zilizopita umetatiza masomo baada ya chuo hicho kufungwa.
Wanafunzi walifanya mgomo wiki jana kutaka kufunguliwa kwa chuo hicho.