Serikali imeahirisha zoezi la kusajili makurutu wa polisi hadi mwaka ujao.
Kwa mjibu wa waziri wa usalama wa taifa Kindiki Kithure amesema zoezi hilo lililopangwa kuandaliwa mwaka huu sasa litafanyika mwaka Mwezi Machi ujao.
Usajili huo unajumuisha ule wa makuruti wa idara ya magereza na wale wa hduma ya kitaifa ya Polisi NPS.
Usajili wa mwisho wa polisi uliandaliwa mwezi Machi mwaka 2022 huku ule wa maregereza ukiandaliwa mwezi April mwaka jana.