Serikali ya Uingereza kutoa pesa za kusaidia walioathiriwa na mafuriko

Marion Bosire
1 Min Read

Serikali ya Uingereza kupitia ubalozi wake nchini Kenya imeahidi kutoa pesa zitakazotumiwa kusaidia watu ambao wameathiriwa na mafuriko katika sehemu mbali mbali nchini.

Pesa hizo ambazo ni milioni 140 zitasambazwa na hazina ya watoto ya Umoja wa Mataifa UNICEF kwa lengo la kutoa usaidizi wa dharura kwa waathiriwa wa mafuriko.

Katika taarifa balozi wa Uingereza nchini Neil Wigan alisema sehemu ya pesa hizo itatolewa kama pesa taslimu kwa familia zipatazo 6,900 ambazo zimeathirika zaidi ili ziweze kurejelea hali ya kawaida.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Kenya Shaheen Nilofer alisema shirika hilo litasimamia usambazaji wa pesa taslimu kwa familia zilizoathirika zaidi.

Kero la mafuriko limesababisha vifo vya takriban watu 228 kuligana na takwimu za serikali ambapo pia watu wapatao 164 wamejeruhiwa huku wengine 212,630 wakipoteza makazi katika sehemu mbali mbali nchini.

Website |  + posts
Share This Article