Serikali ya Tanzania yapanga kuweka lami barabara ya mbugani Serengeti

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Tanzania imeomba kibali kutoka kwa shirika la umoja wa mataifa la UNESCO, ili kuruhusiwa kuweka lami barabara inayopita ndani ya mbuga ya kitaifa ya Serengeti National .

Jaribio la kwanza la serikali kuweka lami barabara hiyo ya umbali wa kilomita 452 itayounganisha Arusha na Musoma hadi ufuoni mwa ziwa Victoria, lilipangwa baina ya mwaka 2005 na 2012 lakini likagonga mwamba.

Kulingana na msemaji wa serikali Mobhare Matinyi ,tayari wamewasilisha mswaada kwa UNESCO kuomba kibali cha kuweka lami barabara hiyo ambayo  imekuwa ikitataiza shughuli za kitalii msimu wa mvua za masika.

Hifadhi ya wanyama ya Serengeti ndio kubwa zaidi nchini Tanzania ikiwa na ukubwa wa kilomita 14,763 mraba na iliorodheshwa kama turathi ya ya UNESCO mwaka 1981.

Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ilitenga dola milioni 480 mwaka 2005 kwa ukarabati wa barabara hiyo, lakiniju hudi hizo zikazimwa na wataalamu wa maswala ya wanayamapori wakihoji kuwa ingetatiza uhamaji wa nyumbu

Share This Article