Serikali ya Kenya yaonya dhidi kupiga marufuku TikTok

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Kenya imetahadahari umma dhidi ya pendekezo la kupiga marufuku mtandao wa TikTok, huku wengi wakitilia shaka ufaafu wake katika jamii .

Serikali badala yake inapendekeza kudhiitiwa kwa taarifa zinazoenezwa kupitia kwa mtandao huo, ili kusiwe na taarifa chafu badala ya kuufungunga.

Kamati ya bunge imekuwa ikidadisi na kujadili malalamishi ya kutaka kufungwa mtandao huo wa China, huku wizara ya usalama wa kitaifa ikihoji kuwa unatumika kueneza propaganda,video chafu na kuwapora Wakenya.

Mtandao huo umekuwa na vikwazo vingi katika mataifa kadhaa Marekani ikidhinisha kuupiga marufu endapo mmiliki wake ByteDance, hataondoa biashara hiyo nchini humo ndani ya mwaka mmoja ujao,wakati Italia ikitia shaka mtandao huo wakati Ufaransa ikiupiga marufuku.

TAGGED:
Share This Article