Serikali ya kaunti ya Tana River imeombwa ikarabati barabara zinazounganisha eneo la Milalulu katika eneo bunge la Galole.
Kulingana na seneta wa kaunti hiyo Danson Mungatana, barabara hizo zinazidi kuwa mbaya hasa wakati wa mvua, na kuwa kikwazo kwa usafiri.
Mungatana alimtaka pia Gavana Dhadho Godhana, kushughulikia suala hilo akidai kwamba amekuwa akilipuuza kwa muda mrefu.
Wakazi wa eneo hilo nao, wameonyesha kutoridhika kwao na hali ya barabara hizo wakisema zimekuwa changamoto kuu hasa wanapopatwa na dharura.
Wanasema matukio kama ya kushughulikia wagonjwa au kina mama wajawazito wanaohitaji kufika hospitali yamefanywa kuwa magumu.