Serikali kuwalipa vijana watakaotunza miti Nandi na Kisii

Marion Bosire
1 Min Read

Serikali kuu kupitia wizara ya mawasiliano na uchumi digitali, imehaidi kuwalipa vijana watakao palilia na kunyunyiza maji miche ya miti inayopandwa katika kaunti ya Nandi na Kisii.

Akizungumza wakati wa zoezi la upanzi wa miche katika msitu wa Kubujo – Nandi Kusini, naibu huyo mkuu wa katibu katika wizara hiyo, Hezron Nyamberi alisema kuwa mpango huo umezaa matunda kaunti ya Kisii na hivi karibuni utazinduliwa Nandi.

“Tulianza kulenga vijana tangu mwezi wa septemba kule Kisii kulinda miche iliyopandwa, hadi sasa, hakuna mti uliongolewa au kuharibiwa kama awali.” Alisema Nyamberi.

Pia alifichua kuwa wizara hiyo inashirikiana na jamii husika Kupata maskauti wa shughuli hiyo huku akirai mashirika ya kibinafsi kushirikiana na wizara hiyo kwa manufaa ya upanzi huo.

Hatua hii inajiri baada ya taarifa kuwa, baadhi ya miche zilizopandwa kote nchini zimo katika hali tete kwa kukosa utunzwaji murwa tangu zoezi hilo kuzinduliwa na rais William Ruto kwa lengo la kuboresha mazingira na mabadiliko ya tabia nchini.

Share This Article