Serikali kuwaelimisha wananchi kuhusu Mswada wa Fedha 2024 ulioondolewa

Tom Mathinji
1 Min Read

Serikali kuu inanuia kuwatumia maafisa wa utawala, kuwaelimisha wananchi kuhusu baadhi ya vipengee vya mswada wa fedha uliotupiliwa mbali ambavyo vinatazamiwa kurejelewa upya.

Haya ni kwa mujibu wa katibu wa mipango ya kitaifa James Muhatia, ambaye amewataka maafisa hao kuhakikisha kuwa wananchi wanapata ripoti kamili kuhusiana na vipengele hivyo.

Katibu wa mipango ya Kitaifa James Muhatia aongoza upanzi wa miti katika msitu wa Geta, eneo bunge la Kipipiri kaunti ya Nyandarua.

Akiongea wakati wa hafla ya upanzi wa miti katika msitu wa Geta katika eneo bunge la Kipipiri, kaunti ya Nyandarua, Muhatia alisema kwamba maafisa hao pia watatakiwa kutia bidii kueneza ujumbe kuhusu sera za serikali mashinani.

Aidha katibu huyo ametoa hakikisho kwamba serikali itawashirikisha vijana katika shughuli ya kitaifa ya upanzi wa miti, kupitia mradi wa Kazi kwa vijana ambao utarejeshwa hivi karibuni.

Share This Article