Serikali imepanga kutumia kikamilifu teknologia ya habari , mawasiliano ili kuimarisha upatikanaji na ubora wa elimu kwa wanafunzi.
Akizungumza alipokutana na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Hewlett-Packard (HP),
Enrique Lores, Waziri wa elimu Ezekiel Machogu alisema teknolojia hiyo imebuni nafasi ambazo serikali inataka kutumia katika kutoa huduma za elimu kwa raia.
Machogu alisema masomo ya mtandaoni yana uwezo wa kuimarisha elimu katika Nyanja zote isipokuwa kuwezesha serikali kutumia habari kuhusu elimu kuongeza
uwekezaji wake katika sekta hiyo.
Machogu alisema serikali itaimarisha uwezo wa wanafunzi na walimu kutumia teknologia ya habari na mawasiliano katika kutekeleza mfumo mpya wa elimu-CBC.
Aliunga mkono ushirikiano baina ya kampuni ya HP na serikali katika utoaji suluhu kwa sekta ya elimu.
Kwa upande wake, Lores alisema kampuni yake ina uwezo wa kutoa msaada wa kiteknolojia unaohitajika katika sekta
ya elimu.