Serikali kutumia shilingi milioni 100 kuwarejesha Wakenya nyumbani kutoka Lebanon

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri wa mambo ya nje Musalia Mudavadi.

Serikali imetenga shilingi milioni 100 kuwahamisha Wakenya walio nchini Lebanon, kutokana na mashambulizi ya majeshi ya Isreal dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah.

Haya yamesemwa na Waziri wa masula ya kigeni Musalia Mudavadi alipofika kwenye bunge la Seneti Jumatano, kujibu maswali kuhusu usalama wa Wakenya walio mashariki ya kati.

Mudavadi ameiambia Senate kuwa hakuna Mkenya yeyote kati ya 26,000, walio mashariki ya kati watakwama kutoka na mzozo wa Israel unaonedelea.

Aliongeza kuwa tayari Wakenya 1,500 wamejisajili katika ubalozi wa Kenya nchini Kuwait wakihitaji msaada wa kuhamishwa.

Mudavadi amesema shughuli ya kuwahamisha Wakenya ilianza tarehe moja mwezi huu.

Share This Article