Serikali kutumia kila mbinu kusuluhisha mizozo ya mpaka kati ya Meru na Tharaka Nithi

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali imeahidi kutumia kila mbinu na rasilimali zote zilizopo kusuluhisha kabisa mizozo ya mpaka kati ya kaunti za Meru na Tharaka Nithi. 

Waziri wa Usalama wa Kitaifa Kithure Kindiki amehusisha mizozo hiyo na utwaaji wa ardhi kwa ulaghai, uuzaji wa ardhi moja kwa watu kadhaa, na uwekaji mipaka usiokuwa halali kuwa chanzo cha mizozo kati ya kaunti hizo.

“Maafisa wa serikali wamepewa maagizo makali kuhakikisha haki inadumishwa wakati wakisuluhisha mizozo ya mpakani, kusuluhisha mizozo ya ardhi kwa usawa na kukoma kuingilia masuala ya maeneo hayo ili kuipendelea jamii yoyote au viongozi wa kisiasa,” almesema Waziri Kindiki.

Aliyasema hayo alipofika mbele ya Kamati Kuu ya Bunge la Seneti kuhusu Uwiano wa Kitaifa, Nafasi Sawa na Utangamano wa Kikanda ili kuangazia uwekaji mipaka kati ya kaunti za Meru na Tharaka Nithi.

Jitihada za kutafuta amani zimeanziishwa katika kaunti hizo mbili na zitaongezwa ili kuzipatanisha jamii zinazoishi katika maeneo husika.

Kindiki ameonya kuwa wanasiasa watakaopatikana wakichochea mizozo ya mpakani watakamatwa na kushtakiwa.

Website |  + posts
Share This Article