Katika juhudi za kuhakikisha ufanisi kwa mpango wa utoaji afya Kwa wote, serikali itaunga mkono kikamilifu utengenezaji wa dawa hapa nchini.
Waziri wa afya Susan Nakhumicha siku ya Alhamisi, alisema watengenezaji wa dawa wa hapa nchini, tayari wamechukuwa asilimia 30 ya shilingi bilioni 160 ya soko la dawa zinazotengenezewa humu nchini.
Akizungumza Jijini Nairobi katika warsha ya utengenezaji na usambaji wa chanjo Africa, Nakhumicha alifichua kuwa, kuimarisha utengenezaji wa dawa humu nchini kumeangaziwa kuwa nguzo muhimu katika undelezji na udhibiti wa mfumo wa afya unaoweza kuhimili mahitaji ya kawaida na Hali za dharura Kama inavyokadiriwa kwenye maono ya 2030.
Kulingana na waziri huyo, taifa hili limeshuhudia maendeleo katika utengenezaji wa dawa halisi za kuzuia homa, pumu, septiki, na antibiology.
“Wentengenezaji wa dawa wa humu nchini kama Revital ambao wanatengeneza sindano na vifaa vya uchunguzi wa afya, wametia fora kimataifa na hata kudhibitishwa na Shirika la Afya duniani-WHO mwaka wa 2023 na wanalenga kuwa wasambazaji wa bei nafuu wa sindano Kwa Shirika la UNICEF.
Tasa Pharma, ambao wanatengeneza chachu za Kuzaa, wana uwezo wa kutengeneza chupa za dawa ya sindano milioni kumi, mifuko minne na chiazi za meno Kila mwaka”
Mafanikio haya, yametajwa na waziri kuwa yenye umuhimu mkubwa kwani yamechangia ukuaji wa bidhha za humu nchini na upatikanaji wa huduma ya afya, kuongezeka Kwa nafasi za kazi na kupungua Kwa bei za bidhaa za afya za humu nchini kutokana na kushuka kwa garama ya uagizaji na usafirishaji na Hali Bora ya kudhiti na na kutibu magonjwa yanapotokea.
Nakhumicha pia aliongeza kuwa, Kwa zaidi ya miaka kumi, bara la Afrika limekumbana na mlipuko wa magonjwa mbalimbali hatari kama vile Ebola, homa ya Rift valley, homa ya Lassa na COVID-19 na humiza haja ya kuekeza katika utengenezaji wa dawa nchini.