Serikali kuongeza mara dufu utoaji pasipoti na vitambulisho

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali inalenga kuongeza maradufu idadi ya pasipoti na vitambulisho itakazotoa kwa Wakenya kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Kulingana na katibu wa idara ya uhamiaji Julius Bitok wataongeza idadi ya pasipoti hadi milioni 1 ifikiapo mwishoni mwa mwaka huu, na kutoa angaa vitambulisho milioni moja.

Serikali pia inapania kuongeza kiwango cha pesa inazokusanya kutokana kwa utoaji huduma hizo kupitia kwa mtandao wa eCitizen, hadi wastani wa shilingi bilioni 1 kwa kila siku.

Bitok amesema haya Ijumaa kwenye kikao cha mipango ya mameneja wakuu na wakurugenzi wanaohudumu katika idara ya uhamiaji, akifafanua kuwa tayari mashine mpya mbili za kuchapisha pasipoti zimewasilishwa katika jumba la Nyayo na zitaunganishwa hivi karibuni.

Serikali pia inalenga kutoa vitambulisho vipya vya kidijitali milioni 1.2 kwa wanaotuma maombi kwa mara ya kwanza, na nakala milioni 1.6 za vitambulisho kuongezea kwa kadi 733,000 za Maisha cards ambazo zimetolewa hadi sasa.

Share This Article