Serikali imejitolea kuongeza fedha zinazotengewa sekta ya afya, huku ikitakiwa kuhakikisha fedha hizo zinatumika ipasavyo kuboresha huduma za afya nchini.
Wakiongozwa na Baraza la Magavana nchini, wadau katika sekta hiyo walitoa wito wa kuongezwa kwa fedha zinazotengewa sekta hiyo ili kuhahikisha kuwa mpango wa huduma bora kwa wote unafanikishwa.
Kwa upande wake, serikali pia imejitolea kuongeza uwekezaji wake katika sekta hiyo kupitia ushuru unaolipwa, mapato yanayotokana na malipo ya bima za kijamii na pia kupitia uwekezaji kutoka sekta ya kibinafsi.
Serikali itashirikiana na sekta ya kibinafsi kuboresha huduma za afya kwa umma na kuwezesha watu wengi kupata huduma hizo.
Mkurugenzi wa ufadhili wa sekta ya afya Dkt. Elizabeth Wanga, alielezea kujitolea kwa serikali kuafikia utoaji huduma bora za afya kwa wote.
Wanga alisema serikali inatambua umuhimu mkubwa wa ufadhili katika sekta ya afya kuhakikisha malengo yake yanatimizwa.