Serikali imeanzisha msako kote nchini Kenya, kukabialiana na wachuuzi wa maziwa ambayo hayajaidhinishwa .
Waziri wa kilimo Mutahi Kagwe ,amesema wamekamata mitambo 25 ya kuhifadhi maziwa katika eneo la Uhuru Park, jijini Nairobi.
Kagwe ameongeza kua maziwa hayo ni hatari kwa usalama na afya ya kwa wanayoyatumia kwani hayajapasishwa,akiapa kumaliza biashara hiyo haramu.
“Uchuuzi wa maziwa ni sharti ukomeshwe.Ni hatari kwa afya na unamaliza uwezo wa kuongeza thamani .”akasema Kagwe
Kagwe alisema mageuzi kadhaa katika sekta ya maziwa yanafanywa, ili kuhakikisha Kenya, inauza maziwa ya thamani na yenye ubora nje ya nchi.