Serikali kujumuisha malipo ya nyumba na afya kwenye NSSF

Martin Mwanje
1 Min Read

Waziri wa Fedha Prof. Njuguna Ndung’u amesema kuwa serikali itaongeza akaunti zingine kwenye mpango wa malipo ya uzeeni, NSSF kwa lengo la kumudu afya na nyumba baada ya kustaafu.

Akiwahutubia wanahabari afisini mwake jijini Nairobi, Prof. Ndung’u alisema kuwa idadi kubwa ya wafanyakazi wa serikali wanastaafu ila mpango wa malipo ya uzeeni hauna uwezo wa kumudu afya na nyumba, jambo ambalo ni changamoto kwa wafanyikazi hao na serikali.

Aliongeza kuwa serikali itaweka mikakati ya kisheria ya akaunti zitakazoundwa ili kuwepo zile za muda mfupi na mrefu kwa lengo la kukimu mahitaji ya mara kwa mara ya fedha.

Mikakati hii pia itazuia wafanyakazi kutumia fedha za uzeeni kabla ya kustaafu.

Katika harakati hizi, wale wanaofanya kazi kwa kandarasi ya muda mfupi pia watajumuishwa.

Kwa sasa, wafanyakazi wa serikali waliostaafu hupewa kiasi kidogo cha pesa kukimu mahitaji yao ya kimsingi kupitia mpango wa NSSF.

Share This Article