Serikali kujenga madarasa 16,000 kote nchini, asema Dkt. Kipsang

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali itajenga madarasa 16,000 kote nchini yatakayotumiwa na wanafunzi watakaojiunga na Gredi ya 9 mwaka ujao.

Katibu wa Elimu ya Msingi Dkt. Belio Kipsang ameyasema haya katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Uratibu na Utekelezaji wa Miradi Elijah Mungai wakati wa halfa iliyoandaliwa katika shule ya msingi ya Olympics mtaani Kibra, kaunti ya Nairobi.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Maendeleo ya Binadamu wa Benki ya Dunia Mamta Murthi miongoni mwa maafisa wengine wa ngazi za juu.

Dkt. Kipsang alisema serikali itajenga madarasa mengine 10 zaidi kwa ajili ya wanafunzi watakaojiunga na Gredi ya 9 mwakani.

“Tunaikaribisha Benki ya Dunia kuunga mkono na kushirikiana na serikali kujenga hata madarasa zaidi katika shule hii,” alisema Dkt. Kipsang.

Murthi aliipongeza Kenya kwa kuwa na matokeo thabiti ya elimu miongoni mwa wanafunzi.

Alisema mfumo wa elimu nchini Kenya unawapa wanafunzi uelewa, ujuzi na maadili ambayo wanapaswa kuwa nayo.

Share This Article