Serikali kujenga mabwawa zaidi kote nchini

Tom Mathinji
1 Min Read
Mabwawa zaidi kujengwa kote nchini.

Baraza la mawaziri limeidhinisha ujenzi wa mabwawa zaidi kote nchini.

Zaidi ya hifadhi 4,000 za maji pia zitakarabatiwa katika mpango mpya wa kuhakikisha usambazaji dhabiti wa maji kote nchini.

Hatua hiyo ambayo inaambatana na ajenda ya kuimarisha uchumi ya Bottom Up, itahakikisha upatikanaji wa maji kwa unyunyiziaji mashamba na pia matumizi ya nyumbani.

Mpango huo utaigharimu serikali kitita cha shilingi bilioni 83, unaojumuisha ujenzi wa mabwawa 25 ya kiwango cha kadri, yatakayohudumia maeneo kame hapa nchini.

Mabwawa hayo yanatarajiwa kusambaza jumla ya lita milioni 353 za maji, na kuhudumia familia   600,000.

Hatua hiyo ya baraza la mawaziri, inajiri huku taifa hili likishuhudia mvua kubwa katika maeneo mengi ya nchini.

Wakati huo huo Baraza hilo la mawaziri limeazimia kutenga siku ya upanzi wa miti, ili kuafikia lengo la serikali la upanzi wa miti bilioni 15.

Hatua hiyo inalenga kuongeza utandu wa misitu hapa nchini, huku kila waziri akihitajika kuongoza mpango huo katika angalau kaunti mbili.

Kenya inalenga kupanda miti bilioni 15 kufikia mwaka 2032.

Share This Article