Serikali kujenga maabara 1600 kote nchini

Naibu Rais Kithure Kindiki alisema hayo wakati wa sherehe ya miaka 120 tangu kuanzishwa kwa shule ya upili ya Jamhuri.

Marion Bosire
2 Min Read
Waziri wa usalama Prof. Kithure Kindiki.

Serikali itajenga maabara 1,600 ya sayansi kote nchini ili kuhakikisha kila shule ina moja.

Haya ni kulingana na Naibu Rais Kithure Kindiki aliyekuwa akizungumza wakati wa sherehe ya miaka 120 tangu kuanzishwa kwa shule ya upili ya Jamhuri.

Kindiki alisema maabara hizo zitafaidi wanafunzi ambao wanapania kusomea Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati almaarufu STEM katika sekondari ya juu.

Naibu Rais Kindiki alisema pia kwamba kufikia sasa, serikali imejenga madarasa elfu 15, ya CBC katika sehemu mbali mbali za nchi na inapanga kuongeza mengine elfu 7,000 katika muda wa mwaka mmoja ujao.

Alithibitisha kujitolea kwa serikali kuajiri walimu elfu 116, katika muda wa miaka mitano ijayo ili kuziba pengo la nguvukazi katika sekta ya elimu.

Kindiki alisema pia kwamba ni muhimu kuendeleza ubora wa vizazi ili kuimarisha maadili ambayo ni sehemu muhimu ya shughuli za nchi huku akisisitiza kwamba kuna watu wazima wa kutosha ambao ni mfano wa kuigwa na vijana.

Jamii ya wanafunzi wa zamani na walimu wa Jamhuri imeanzisha mpango wa kuchangisha shilingi milioni 120 katika muda wa siku 120, fedha ambazo zitatumika kwa ujenzi wa miundombinu na kugharamia masomo ya wanafunzi.

Sehemu ya pesa hizo zitatumiwa pia kujenga kituo cha kidijitali shuleni humo kati ya miradi mingine.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *