Serikali kuanza kusambaza mbolea kesho asema Kagwe

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali itaanza usambazaji wa mifuko milioni moja ya mbolea ya bei nafuu kwa wakulima kesho tayari kwa msimu wa upanzi.

Waziri wa kilimo na ustawishaji wa mifugo Mutahi Kagwe, amesema tayari shehena za mbolea hiyo zimesafirishwa kutoka Mombasa hadi Naivasha .

Mbolea hiyo itasambazwa kupitia kwa maghala ya halmashauri ya nafaka na mazao nchini  NCPB,kabla ya kugawiwa wakulima.

Aidha, serikali imewaonya wakulima dhidi ya kununua mbolea kutoka kwa madalali ambao hawajasajiliwa ambao wengi wao huuza mbolea ghushi.

Website |  + posts
Share This Article