Serikali kuwaajiri wanagenzi 3,752 wa afya kote nchini

Tom Mathinji
1 Min Read

Serikali imewaandikia barua zaidi ya wanagenzi 1,000 wa afya kote nchini, ikiwataka kufika kwenye vituo vya kazi kuanzia mwezi ujao.

Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa utawala wa wizara ya afya Adan Harakhe.

Katika mpango huu serikali inalenga wanagenzi 3,752 wanaojumuisha maafisa wa kliniki walio na diploma 1,270, na 1,125 wa shahada, daktari wa meno 73, Mafamasia 290 na maafisa wa matibabu 849.

Adan ameongeza kuwa wizara hiyo imo mbioni kuangazia upya sera za wanagenzi kwa lengo la kuwapa kazi mwisho wa muda wa kuhudumu.

Kwa sasa, madaktari wanagenzi walio na diploma watalipwa shilingi 25,000 kutoka 15,000 za hapo awali.

TAGGED:
Share This Article