Waziri wa Usalama wa Kitaifa Kithure Kindiki amesema kuwa serikali imefunga maeneo ya kuuza pombe 9,269, tangu mwezi Machi mwaka huu. Hii katika msako ambao unaendeshwa dhidi ya baa ambazo hazijazingatia sheria.
Ufungaji wa baa hizo ulitekelezwa kati ya Machi 8 na 31 huku vituo 150 vya kuuza shisha vikifungwa.
Waziri Kindiki alipiga marufuku matangazo kupitia vyombo vya habari kueneza matumizi ya shisha.
Serikali imezindua msako mkali unaolenga kukabiliana na uuzaji wa pombe haramu ambao umesababisha vifo vya watu wengi nchini hasa eneo la Mlima Kenya.