Serikali imeahirisha ufunguzi wa shule kwa muda usiojulikana

Tom Mathinji
1 Min Read
Wanafunzi wa shule ya upili ya Kiaga.

Rais William Ruto ameagiza wizara ya elimu kuahirisha ufunguzi wa shule kwa muhula wa pili, kwa muda usiojulikana.

Akihutubia taifa leo Ijumaa, Rais alisema hatua hiyo ni kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi yanayoshuhudiwa hapa nchini kutokana na mvua kubwa inayonyesha.

Kulingana na takwimu za serikali siku ya Ijumaa, shule 1,967 zimeaharibiwa na mafuriko na haziwezi tumiwa na wanafunzi kwa masomo.

Aidha kiongozi wa taifa amewataka wabunge wa taifa, kutumia fedha za ustwawishaji maeneo bunge NG-CDF, kukarabati shule ambazo zimeharibiwa na mafuriko.

“Natoa wito kwa wabunge, kutumia fedha za hazina ya ustawi wa maeneo bunge, kukarabati shule zilizoharibiwa na mafuriko,’ alisema Rais Ruto.

TAGGED:
Share This Article