Serikali haitaingilia shughuli za taasisi huru, asema Naibu Rais Rigathi Gachagua

Tom Mathinji
1 Min Read

Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema serikali kuu haina mipango ya kuingilia kazi za taasisi huru nchini.

Akizungumza wakati wa mkutano na tume za kikatiba pamoja na taasisi huru mtaani Karen, Nairobi, Gachagua alisema serikali ya Kenya Kwanza itaendelea kuheshimu kazi za taasisi huru nchini.

“Hatuna lengo la kuingilia majukumu na shughuli zao kikatiba. Hatutavuruga uhuru wao kwa kuwa nchi huwa thabiti sawia na taasisi zake. Tutaheshimu maamuzi ya taasisi hizo,” alisema Naibu Rais.

Gachagua ambaye alikuwa amepewa jukumu la kuwa kiungo baina ya serikali na taasisi hizo na Rais William Ruto, alisema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hizo ili kuhakikisha changamoto zinazokabili utendakazi wake zimekabiliwa vilivyo.

Vilevile aliomba taasisi hizo kutafuta njia mwafaka za kusuluhisha mizozo ili kuwaepushia walipa ushuru ada ya juu wanayotozwa kisheria.

Aidha,  alisema serikali imeongeza mgao wa idara ya mahakama kutoka shilingi bilioni 18 hadi bilioni 22, ili kufanikisha miradi yake bila ufisadi ama uhuru wake kuingiliwa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *