Serem na Kiprop washinda fedha na shaba Michezo ya Afrika

Dismas Otuke
1 Min Read

Amos Serem na Simon Kiprop walinyakua nishani za fedha na shaba mtawalia katika fainali ya mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji, katika siku ya kwanza ya Riadha katika  Michezo ya Afrika inayoendelea mjini Accra ,Ghana.

Serem ambaye ni bingwa wa zamani wa dunia kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20, alimaliza wa pili kwenye fainali hiyo ya Jumatatu usiku akitumia dakika 8 na sekunde 25.77,huku Kiprop akiridhia medali ya shaba kwa dakika 8 sekunde 26.19.

Samuel Firehu Fiche wa Ethiopia alitwaa dhahabu kwa dakika 8 sekunde 24.30.

Mshikilizi wa rekodi ya dunia a mita 3,000 kuruka viunzi na maji Beatrice Chepkoech, alimaliza wa nne katika fainali ya mita 5,000 ,akitumia dakika 15 sekunde 4.32 .

Ethiopia ilinyakua nushani zote tatu,Eisa Kumanda,Molla Birtukan na Melkanut Shaarew wakifuatana katika nafasi za kwanza,pili na tatu mtawalia.

Share This Article