Sepp Blatter aondolewa kesi ya ufisadi

Bonface Mutsotso
1 Min Read

Mahakama ya Rufaa ya uswizi imewaondolea tena mashtaka aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Sepp Blatter na aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Kandanda barani Ulaya ( UEFA) na Meneja wa Timu ya Taifa ya ufaransa Michel Platini. 

Hii ni baada ya wawili hao kushtakiwa mwaka wa 2015 kwa ubadhirifu wa dola milioni mbili.

Ubadhirifu huo ulidaiwa kufanyika wakati Blatter alipokuwa Rais. Anadaiwa kumuru FIFA kumlipa Michel kima hicho kama malipo ya ushauri kwa rais huyo wa zamani tangu mwaka wa 1998 – 2002.

Hali hiyo ilisababisha wawili hao kupoteza nafasi zao za kazi na kufunguliwa mashtaka.

Hata hivyo, mwaka wa 2022, waliachiliwa na mahakama ya chini nchini humo baada ya kukana kosa hilo ila mwendesha mashtaka akakata rufaa.

Bonface Mutsotso
+ posts
Share This Article