Bunge la Seneti mapema Jumatatu limeanza vikao vya kusikiza mashtaka dhidi ya Gavana wa Meru Kawira Mwangaza.
Gavana huyo ambaye ameng’atuliwa afisini kwa mara ya tatu sasa, anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya matumizi mabaya ya afisi.
Mwangaza aliachwa gizani baada ya kufurushwa kupitia kwa kura ya waakilishi wadi wa bunge la kaunti hiyo ,MCA 49 wakitaka apigwe kumbo, huku 17 pekee wamuunga mkono.
Maseneta watasikiza upande wa mashtaka na upande wa Gavana baina ya Jumatatu na Jumanne ,kabla ya kutoa uamuzi.
Gavana Mwangaza anakabiliwa na mashtaka ya ukiukaji wa katiba na sheria nyingine ,matumizi mabaya ya ofisi na kutotekeleza mapendekezo ya bunge la kaunti miongoni mwa makosa mengine.