Bunge la seneti litajadili hoja ya kumuondoa mamlakani Gavana wa Kericho Eric Mutai juma lijalo.
Seneti imetenga Oktoba 14 na 15, kuwa tarehe za kusikiza hoja hiyo, baada ya bunge la kaunti ya Kericho kupiga kura kumuondoa wadhifani.
Vikao hivyo vitaandaliwa licha ya Mahakama kuzuia kujadiliwa kwa hoja hiyo katika bunge la Seneti, hadi keshi iliyowasilishwa katika mahakama kuu ya Kericho itakaposikizwa na kuamuliwa.
Aidha kulingana na maagizo hayo ya mahakama, Mutai ataendelea kutekeleza majukumu yake ya Gavana hadi keshi yake itakapoamuliwa.
Mutai alibanduliwa baada ya wawakilishi wadi 31 kati ya 47 kuunga mkono hoja hiyo iliyowasilishwa na mwakilishi wa wadi ya Sigowet Kiprotich Rogony.
Rogony alitaja sababu nne ambazo ni ukiukaji wa katiba na sheria zingine, ukiukaji wa sjheria mbalio mbali za kitaifa na kaunti, matumizi mabaya ya mamlaka na utovu wa nidhamu.