Seneta Mandago taabani baada ya DPP kuidhinisha ashtakiwe

Dismas Otuke
1 Min Read

Seneta wa Uasin Gishu Jackson Mandago amejipata taabani baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) kuidhinisha mashtaka mapya katika sakata inayomkabili ya shilingi milioni 50 za ufadhili wa masomo ya ughaibuni nchini Finland.

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Renson Ingonga amewasilisha mashtaka mapya baada ya Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI kukosa kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi nchini, EACC imekuwa ikichunguza sakata hiyo ya mpango wa msaada wa masomo wa kaunti ya Uasin Gishu ya kima cha shilingi bilioni 1.1 nchini Finland.

Sakata hiyo ilitokea wakati Mandago akiwa Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu.

Mashahidi 26 tayari wametoa ushahidi huku wengine 12 wakijiondoa.

Washukiwa hao saba akiwemo Mandago wanakabiliwa na kesi ya kushirikiana kutekeleza uhalifu, matumizi mabaya ya afisi na kupokea pesa kwa njia ya utapeli.

Share This Article