Seneta wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago anatarajiwa kufikishwa mahakamani Nakuru leo Alhamisi, Agosti 17, kujibu mashtaka kadhaa ya ufisadi.
Mandago na wenzake wawili wanakabiliwa na mashtaka ya wizi wa shilingi bilioni 1 nukta 1 kwenye sakata ya masomo ya wanafunzi wa Kenya nchini Finland.
Mandago alikamatwa jana Jumatano akiwa nyumbani kwake na kupelekwa katika afisi za polisi wa ujasusi kaunti ya Nakuru alikofungiwa.
Kutiwa mbaroni kwa seneta huyo kulijiri saa chache baada ya Rais William Ruto akiwa kwenye ziara mjini Eldoret kusema kuwa wote waliopora pesa kutoka kwa wazazi kwenye sakata hiyo watawajibishwa kisheria.