Senegal watashuka katika uwanja wa Nelson Mandela, kukabiliana kwa mechi ya kuwania nafasi ya tatu na nne leo katika uwanja wa Nelson Mandela jijini Kampala, Uganda.
Teranga Lions walipoteza katika nusu fainali dhidi ya Morocco, kupitia penati kufuatia sare ya 1-1, huku Sudan wakishindwa kwa bao moja kwa sifuri na Madagascar katika semi fainali.
Aidha, pambano hilo litakuwa marudio ya mechi ya kundi D timu hizo zilipotoka sare ya bao moja.
Fainali ya makala ya nane ya kipute cha CHAN itasakatwa kesho katika uwanja wa Kasarani kuanzia saa kumi na mbili jioni kati ya Morocco na Madagascar.