Bunge la Senate limekataa kuahirisha vikao vya kusikiza hoja ya kumbandua Naibu Rais Rigathi Gachagua hadi siku ya Jumamosi, baada ya Gachagua kukosa kufika katika kikao cha Alhamisi alasiri.
Maseneta hao walipiga kura kuamua iwapo vikao vya Alhamisi alasiri vitaendelea au la, bila kuwepo kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, huku Maseneta wengi wakipiga kura kuunga mkono kuendelea kwa vikao hivyo.
Kingi alikuwa ameagiza kuwa bunge la Senate, liahirishe vikao vyake vya Alhamisi alasiri hadi siku ya Jumamosi, agizo ambalo limepingwa na maseneta.
Wakili wa Gachagua Paul Muite, alisema mteja wake hatafika katika bunge la Senate kwa sababu anaugua.
“Nimeasiliana na madaktari wanaomtibu, lakini sijawasiliana naye moja kwa moja kutokana na hali yake,” alisema Muite.
Muite alikuwa ameomba bunge la Senate kumpa Gachagua fursa ya kujieleza kabla ya zoezi la upigaji kura kuanza.