Sehemu ya barabara ya Nairobi-Mombasa kufungwa

Tom Mathinji
1 Min Read

Halmashauri ya kusimamia barabara kuu nchini (KeNHA), imetangaza kufungwa kwa sehemu kadhaa za barabara ya Nairobi – Mombasa, kutoa nafasi ya ukarabati kuanzia Jumanne Oktoba 29, 2024.

Kupitia kwa ilani kwa umma, KeNHA ilisema ukarabati huo utakaokamilika Novemba 22, 2024, utaathiri maeneo yaliyokaribu na hoteli ya Panari katika barabara hiyo Mombasa.

Baadhi ya ukarabati utakaofanywa ni pamoja na ujenzi wa daraja la kuvuka kwa miguu, kati ya barabara ya Mombasa na ile ya Expressway.

KeNHA imewaonya madereva kuwa huenda eneo hilo litashuhudiwa msongamano  wa magari, huku wakishauriwa kutumia barabara mbadala.

Hata hivyo, kwa mujibu wa halmashauri hiyo, maafisa wa polisi wa trafiki na wale wa kaunti, watawaelekeza madereva wakati wa kipindi hicho cha ukarabati.

TAGGED:
Share This Article