Sean ‘Diddy’ Combs akamatwa New York City

Tom Mathinji
1 Min Read

Mwanamuziki maarufu wa hip-hop Sean “Diddy” Combs amekamatwa katika jiji la New York kwa mashtaka ambayo hayajabainishwa.

Kukamatwa kwa Diddy Manhattan kunafuatia uvamizi wa mali zake mbili huko Los Angeles na Miami mnamo Machi kama sehemu ya “uchunguzi unaoendelea” wa mamlaka kuhusiana na biashara ya ngono.

Wakili wa Bw Combs, Marc Agnifilo, alisema “wamekatishwa tamaa” na kukamatwa huku mteja wake alikuwa “mtu asiye na hatia”.

Mwanamuziki huyo amekabiliwa na msururu wa tuhuma za unyanyasaji wa kingono na unyanyasaji, ikiwa ni pamoja na tuhuma za kumnyanyasa mpenzi wake wa zamani Casandra “Cassie” Ventura. Sheon amekana madai yote dhidi yake.

Alikamatwa kuhusiana na uchunguzi unaoendelea na maafisa wa usalama wa ndani wa Marekani, vyanzo vingi vya sheria viliiambia CBS.

Mwanasheria wa Marekani katika Wilaya ya Kusini ya New York Damian Williams alithibitisha kukamatwa kwake katika taarifa yake Jumatatu usiku.

Share This Article