Saudia imeahirisha kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya Stephen Munyakho

Tom Mathinji
1 Min Read
Stephen Munyakho (Kulia) na mamake Dorothy Kweyu (Kushoto)

Saudi Arabia imekubali kuahirisha kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya raia wa Kenya Stephen Munyakho, iliyotarajiwa kutekelezwa Mei 15,2024, ili kutoa fursa kwa mashauriano zaidi kati ya pande zote husika.

Kupitia kwa taarifa, katibu katika wizara ya mambo ya nje Korir Sing’Oei, alisema Kenya itashiriki meza ya mazungumzo na wadau Jijini Nairobi na Riyadh, pamoja na wawakilishi wa kidini, kukubaliana kuhusu hatua itakayochukuliwa.

Aidha Sing’Oei alisema Kenya itaendelea kuegemea urafiki dhabiti uliopo na washirika wa Saudia, huku serikali hizo mbili zikilenga kutatua swala hilo.

Stephen Munyakho ni mwana wa mwanahabari mkongwe Dorothy Kweyu.

Kweyu amekuwa akiomba usaidizi kutoka kwa watu wenye nia njema, kukusanya shilingi milioni 150, ili kuwezesha mwanawe kuachiliwa huru kabla ya Mei 15,2024 ambayo ndio ilikuwa siku ya kutekelezwa kwa hukumu ya kifo dhidi ya Munyakho.

Stephen Munyakho amekuwa korokoroni kwa muda wa miaka 13. baada ya kuhukumiwa kifo kwa mauaji ya raia wa Yemen.

Alipelekwa jela Aprili 9,2011, na kuzuiliwa katika gereza la Shimeisi,Mecca Saudi Arabia.

Share This Article