Saudi Arabia yaangusha droni mbili mjini Riyadh

Dismas Otuke
1 Min Read

Saudi Arabia imesema imeangusha droni mbili katika mji mkuu wa Riyadh mapema Ijumaa.

Wizara ya ulinzi nchini Saudi Arabia imesema jeshi lake la anga lilitungua na kuharibu droni mbili zilizokuwa zikielekea Riyadh.

Lilikuwa shambulizi la pili chini ya lisaa limoja karibu na mji mkuu wa Saudia ,Riyadh .

Katika shambulizi la kwanza siku ya Alhamisi, droni mbili ziliangushwa na majeshi ya Saudia huku nyingine nne nne zikianguka baharini.

Share This Article